MBIBO Azungumza na Ujumbe Kutoka Urusi.
GST kushirikiana na Federal Agency For Minerals Resources of the Russian Federation Utafiti wa Madini
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo ametoa wito kwa Wawekezaji kuchangamkia fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini ikiwemo kuwekeza kwenye kufanya tafiti za Jiolojia kwa kutumia Teknolojia ya Kisasa ili kuvumbua maeneo mapya ya uchimbaji madini.
Mbibo amesema hayo leo Oktoba 29, 2024 alipokutana na kuzungumza na ujumbe kutoka Federal Agency for Minerals Resources of Russian Federation Jijini Dar es salaaam uliyokuwa ukishiriki Mkutano wa Tanzania-Russiaan Business and Investment Forum.
Katika Mazungumzo hayo, Mbibo amesisitiza umuhimu wa kuwepo kwa Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya Federal Agency for Minerals Resources of the Russian Federation na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ili kuleta tija katika tafiti za pamoja.
Katika hatua nyingine, Mbibo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Uendelezaji Biashara akiwakilisha Sberbank International katika Ukanda wa Subsaharan Afrika ili kuangalia uwezekano wa kushiriki katika kufadhili miradi ya Utafiti na uchunguzi wa majanga ya Jiolojia ikiwemo Matetemeko ya ardhi, kububujika kwa tope, mafuliko nk.
Aidha, Mbibo amesema, Tanzania ni nchi salama kwa uwekezaji na kuusisitiza ujumbe huo kuwekeza kwenye kufanya Utafiti wa Jiolojia kwa kutumia Teknolojia ya Kisasa ili kubaini maeneo mapya yenye viashiria vya madini.
Kwa upande wake, Andrey Vorobieve ambeye pia ni kiongozi wa Ujumbe huo, amemhakikishia Naibu Katibu Mkuu kwamba mambo yote waliyozungumza katika mazungumzo Yao na yaliyozungumzwa kwenye Mkutano wa siku mbili yote yatatekelezeka kupitia mashirikiano.
Aidha, kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha wataalamu kilichofanyika Oktoba 28, 2024 ambacho pia Naibu Katibu Mkuu alishiriki pamoja na Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Budeba Mtendaji Mkuu GST.