Taarifa kwa Umma kwa Wamiliki wa Leseni za Utafiti na Uchimbaji wa Madini

Wakala wa Jiolojia Tanzania (Geological Survey of Tanzania - GST) inawakumbusha wamiliki wote wa Leseni za Utafiti na Uchimbaji Madini kuwasilisha takwimu na taarifa za utafiti/uchimbaji wa madini nchini.

Uwasilishwaji wa taarifa/takwimu hizo ni kwa mujibu wa vifungu vya Sheria ya Madini, Kifungu cha 27F (3) na (4) cha Sheria ya Madini Na. 14 ya Mwaka 2010 kama ilivyorekebishwa na ʺThe Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act No. 7, 2017ʺ. Vifungu hivyo vinaelekeza kama ifuatavyo:
27F.-(3) The mineral right holder shall submit to the Geological Survey of Tanzania the following accurate mineral data:
(a) geological maps and plans;
(b) geophysical and geochemical raw data;
(c) processed and interpreted data or maps;
(d) technical reports;
(e) core samples and its mineral exploration database; and
(f) any other information as may be required.
(4)The mineral right holder shall give copies of data generated under subsections (2) and (3) to the Geological Survey of Tanzania free of charge.

Kutokana na sheria hii, ni lazima taarifa hizi ziwasilishwe Geological Survey of Tanzania (GST) kila baada ya miezi mitatu (quarterly basis) kuanzia Oktoba 2017.

Imetolewa tarehe 10 Januari 2018 na:

Mtendaji Mkuu,
Wakala wa Jiolojia Tanzania,
Mtaa wa Kikuyu, Jengo Na.8
S.L.P 903, DODOMA,
TANZANIA.

Simu: +255 26 2323020/0754497533
Nukushi: +255 26 2323020
Barua pepe: madini.do@gst.go.tz
Tovuti: http:www.gst.go.tz
Portal: www.gmis-tanzania.com