TAARIFA KWA UMMA KUHUSU TETEMEKO LA ARDHI

Mnamo tarehe 25/3/2018 majira ya saa 6:18 usiku kulitokea tetemeko la ardhi mkoani Shinyanga lenye ukubwa wa 4.6 katika kipimo cha Richter. Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa umbali wa kilomita 6.2 kusini magharibi mwa mji wa Lungunya na kilomita 47 Mashariki ya mji wa Ushirombo katika Latitudo -3.434 na Longitudo 32.384. Mtikisiko wa ardhi uliosababishwa na tetemeko hilo ulisikika katika maeneo ya mkoa wa Shinyanga, Geita, Kagera, Simiyu, Mwanza, Tabora na hata nchi jirani za Kenya na Uganda. Mpaka sasa kuna taarifa za athari za tetemeko hilo ambapo baadhi ya watu wamejeruhiwa ikiwa ni pamoja na majengo kubomoka katika Wilaya ya Mbogwe.

Download

Read