TAARIFA KUHUSU TETEMEKO LA ARDHI LILILOTOKEA MKOANI GEITA TAREHE 25/5/2017

Mnamo tarehe 25 Mei 2017 majira ya saa 06:55:28.29 mchana kulitokea tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 4.4 katika kipimo cha Richter ambalo lilisikika katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Geita ikiwa ni pamoja na maeneo ya Mwanza, Shinyanga, Ushirombo, Uganda na Kenya. Kitovu cha tetemeko kilikuwa kilomita 1.5 Kusini Magharibi ya kijiji cha Lukanga kwenye Latitudo -3.054 na Longitudo 32.893 katika kina cha kilomita 10 kutoka uso wa ardhi. Tetemeko hilo lilizua hofu na taharuki kubwa kwa wakazi wa mkoa wa Geita, Shinyanga na baadhi ya maeneo ya mji wa Mwanza ambapo lilisababisha kifo cha mtu mmoja (askari polisi) katika mji wa Mwanza kutokana na kupatwa na mstuko. Aidha watu wengine 18 walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini ambao ni wanafunzi wa shule za sekondari katika Wilaya ya Nyanghwale. Wanafunzi hao walipata madhara kutokana na taharuki iliyosababisha wakanyagane milangoni wakati wakijaribu kukimbia kutoka ndani ya vyumba vya madarasa.

Download

Read